Jumanne , 25th Nov , 2014

Shirikisho la soka nchini TFF limesema linasubiri programu ya kocha wa Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afrika All Africa Games itakayofanyika hapo mwakani Congo Brazzaville.

Akizungumza jijini Dar es es salaam,Mkurugenzi wa mashindano wa TFF,Boniface Wambura amesema michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Machi mwakani,Tanzania itaanza mechi yake ikicheza dhidi ya Zambia.

Wambura amesema kocha yupo katika maandalizi ikiwa ni sehemu ya kuiwekea timu hiyo nafasi kwa ajili ya kuweza kufanya vizuri katika michuano hiyo.