
Mlinda mlango wa Yanga Dida akiwa golini kusubiri mpira ambao unawaniwa na beki wa Yanga, Mbuyu Twite aliyeruka juu kupiga mpira kwa kichwa dhidi ya Jean Kasusula wa TP Mazembe
Dida amesema, mchezo ulikuwa mzuri na TP Mazembe imecheza ikiamini imekutana na Yanga ambayo inauwezo wa kupambana ili kuweza kusonga mbele zaidi.
Dida amesema, wao walijipanga na hata wapinzani wao pia walijipanga kwa ajili ya mchezo huo lakini makosa yaliyotokea ndio yalisababisha wapinzani wao kuweza kupata ushindi katika mchezo huo.
Yanga ilikubali kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa TP Mazembe hapo jana bao lililowekwa nyavuni na Mereveille Boppe aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Chrtistian Luyindama katika dakika ya 74.