
Mkurugenzi wa TPLB Boniface Wambura amesema, Timu ya Taifa inatengenezwa kwa kupitia kwenye ligi kama ilivyo kwa nchi mbalimbali hususani Algeria lakini wana wachezaji wengi wanaocheza nje ya ligi ambayo kwa upande wao ni faida.
Wambura amesema, kwa upande wa Tanzania kuna wachezaji wachache ambao wanacheza ligi za nje suala lililochangia hata hapo jana kuweza kupata matokeo mabaya dhidi ya Algeria.
Kwa upande wake, beki wa pembeni aliyekuwa akiitumikia Klabu ya Simba ambaye kwa sasa anaitumikia timu ya Neckarsulmer ya nchinu Ujerumani Emily Mgeta amesema, Tanzania imeshakosa nafasi hivyo wanatakiwa kujipanga upya kwa kuwa na kikosi cha timu za vijana ambao watawezesha kukuza soka la hapa nchini.
Emily amesema, mpira hauna njia ya mkato hivyo inatakiwa kujipanga kwa kukuza vipaji vya soka kwa vijana ambao hapo baadaye watakuwa ni faida kwa nchi.