Ijumaa , 27th Mar , 2015

Chama cha mchezo wa Tennisi Nchini TTA kinatarajia kufanya uchaguzi wa Rais wa Chama hicho hivi karibuni ili kumaliza kabisa migogoro iliyokuwa ikiendelea kati ya viongozi wa vilabu na viongozi wa TTA.

Akizungumza na East Africa Radio, Mjumbe wa TTA, Hassan Kassim amesema, mgogoro ulikuwa ukisababishwa na kutokuwa na uwazi wa Taarifa katika Chama hicho, suala lililozua migogoro katika Chama hicho na kupelekea kushindwa kuendesha mashindano ya mchezo wa Tenisi hapa nchini.

Kassim amesema, licha ya kufanya uchaguzi pia Chama hicho kinatakiwa kuwa na uzalendo kwa kumjali kila mdau wa mchezo huo ili kuuendeleza na kuukuza mchezo huo hapa nchini.