Jumatano , 11th Nov , 2015

Uongozi mpya wa chama cha kuogelea nchini TSA umesema wameshakaa vikao kwa ajili ya kuunda kamati kuhusiana na marekebisho ya katiba iliyoagizwa na Baraza la Michezo Tanzania BMT.

Katibu mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema, kamati hiyo ina watu watano, wanne wakitokea Tanzania Bara na mmoja akitokea Zanzibar kama ilivyoagizwa na wamekwishachagua katibu na mwenyekiti wa kamati.

Namkoveka amesema, Novemba 28 rasimu ya kwanza ya katiba ya chama hicho wataipokea kutoka kwa kamati ambapo wataisambaza kwa wadau ili waweze kutoa mapendekezo yao ili Katiba pendekezwa iweze kupitishwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kwanza mwakani.