Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu nchini TAVA, Muharame Mchume amesema timu hiyo itakayokuwa chini ya kocha Nassoro Sharifu, inatarajia kuingia kambini ikiwa na jumla ya wachezaji 12 ambapo ni sita wakiume na sita wakike japo katika michuano hiyo watatumika wachezaji wanne.
Mchume amesema, wameamua kuwa na vijana wengi kambini kwa ajili ya dharura mbalimbali zitakazojitokeza katika michuano hiyo.
Mchume amesema, timu shiriki katika michuano hiyo ambazo ni Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti zinatarajiwa kuwasili nchini Fabruari 15 kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 16 hadi 18 katika fukwe za jijini Dar es salaam.