Katibu mkuu wa chama cha judo Tanzania JATA Innocent Malya amesema, mashindano hayo hayatawashirikisha wachezaji kutoka Zanzibar kwa kuwa yanalenga kutafuta timu ya Tanzania Bara.
Malya amesema, mpaka sasa kamati ya mashindano ya JATA haijapanga tarehe maalumu ya kuanzia ingawa wamependekeza yafanyike Desemba mwaka huu.
Malya amesema, wachezaji watakaochaguliwa kuunda timu ya taifa wataanza mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kufanyika Februari mwakani nchini Burundi.