Baadhi ya majukwaa ya uwanja wa Taifa
Kwa mujibu wa taarifa hiyo jumla ya mashabiki 13,782 ndiyo watakaopaswa kukata tiketi mpya kwa sababu katika mchezo uliyohairishwa 8 mei 2021 wale waliokata tiketi kwa mfumo wa NCARD hawatalazimika kulipa tena.
Mgawanyiko wa tiketi 13,782 kama ufuatavyo tiketi 2,218 ni za jukwaa la kijani ( mzunguko) tiketi 11,280 ni za jukwaa la machungwa (orange) na tiketi 284 VIP B taarifa imesisitiza hakutakuwa na tiketi za VIP A na C zitakazouzwa kwa ajili mchezo huo wa julai 3
Viingilio vimepangwa kama ifuatavyo mzunguko shilingi 7,000, machungwa 10,000 na kwa upande wa VIP B kiingilio ni 20,000
Simba na Yanga wanakutana baada ya mchezo wao wa tarehe 8 mei kuhairishwa kufuatia sintofahamu iliyozuka baada ya muda wa mchezo kusogezwa mbele, uwanja wa taifa unachukua mashabiki 60,000
