Alhamisi , 4th Dec , 2014

Shirikisho la Soka nchini TFF, linatarajia kukutana na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga vinavyoshiriki mechi ya Nani Mtani Jembe inayotarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema lengo la kukutana na viongozi hao ni kuwakumbusha taratibu za mechi pamoja na sheria mpya zilizopo katika mechi hiyo.

Wambura amesema katika mechi hiyo wachezaji wa timu mojawapo ambayo haikuibuka mshindi wanatakiwa kubaki uwanjani wakati wa ugawaji wa zawadi na iwapo timu haitabaki kushuhudia zoezi hilo itachukuliwa sheria.