
Baada ya hivi karibuni kikosi hicho kuwakosa nyota wake watatu ambao ni Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Mzimbabwe, Donald Ngoma kutokana na majeraha, pia kitamkosa kiungo wake kiraka, Salum Telela kwa zaidi ya wiki mbili.
Katika taarifa yake daktari wa Yanga Haruni Ally amesema, Telela atakuwa nje ya uwaja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu yaliyokuwa yakimsumbua mara kwa mara na kumfanya ashindwe kucheza soka kama inavyotakiwa.
Dkt Haruni amesema, baada ya kumfanyia vipimo vya MRI waligundua Telela ana tatizo kubwa ambalo litamfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo