Ijumaa , 30th Jul , 2021

Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 imetwaa ubingwa wa michuano ya CECAFA U-23 Challenge CUP 2021, baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 6-5 dhidi ya timu ya taifa ya Burundi mchezo uliochezwa katika dimba la Bahir Dar Ethiopia.

Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23

Mchezo huu wa finali ulifika hatua ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya timu hizi kutofungana ndani ya dakika 90, na timu zote zilipiga penati 6 na Tanzania ikafanikiwa kufunga penati zote na Burundi wakakosa moja na kuifanya Tanzania kuwa mabingwa wakiwavua ubingwa Uganda ambao walikwa mabingwa watetezi.

Tanzania ilitinga fainali kwa kuitoa timu ya taifa ya Sudan Kusini kwa kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali wakati Burundi walifuzu hatua ya fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Kenya baada ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu ndani ya dakika 90.

Michuano hii ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ukanda wa Afrika mashariki na kati imefanyika nchini Ethiopia na ilijumuhisha jumla ya timu tisa (9) nane kutoka ukanda huu ambazo ni Burundi, Tanzania, Kenya, Sudani Kusini, Ethiopia, Eritrea, Uganda, na Djbout na timu ya taifa ya Jamuhuri ya Kidemokaria ya Kongo ilishiriki kama timu waarikwa.