Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Tamko la Namungo kwa wachezaji waliobaki Angola

Alhamisi , 25th Feb , 2021

Mwenyekiti wa klabu ya Namungo, Hassan Zidadu amesema wachezaji watatu na kiongozi mmoja wa klabu hiyo waliokwama nchini Angola baada ya kukutwa na maambukizi ya Covid-19 wameachiwa huru na tayari wameshaanza taratibu za kuwarudisha nchini.

Wachezaji wa Namungo wakishangilia moja ya bao kwenye mchezo wake uliopit dhidi ya Primeiro de Agosto, jumapili iliyopita.

Zidadu amesema :

“Tulikuwa tunawasiliana nao kila siku, asubuhi, mchana na jioni. Lakini serikali ya Angola ilisema itawaachia wakiwapima na kujiridhisha kama hawana maambukizi. Tunashukuru Mungu kwa mujibu wa vipimo vyao jana asubuhi na majibu kutoka mchana, hawana maambukizi na wameachiwa huru”.

“Tunasikitika kwasababu serikali ya Angola iliahidi gharama za kuwasafirisha lakini leo imejitoa na badala yake inabidi sisi tuwasafirishe wenyewe na tumeshaanza utaratibu huo. Watarejea nchini kati ya Jumamosi au Jumatatu”.

Ikumbukwe, Wanne walikutwa na maambukizi wakati Namungo ilipowasili nchini Angola kwa ajili ya  kucheza dhidi ya Premiero de Agsoto ya nchini humo kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shrikisho barani Africa.

Baada ya Skata hilo, Shirikisho la soka barani Afrika 'CAF', liliamua kuufuta mchezo huo na siku chache baadaye ukapangwa uchezwe nchini Tanzania.

Wawili hao wamekipiga siku ya Jumapili ya tarehe 21 Februari mwaka huu katika dimba la Chamazi na Namungo kuibuka na ushindi wa mabao 6-2 ikihesabiwa kama mchezo wa ugenini dhidi ya timu hiyo ya nchini Angola.

Mchezo wa mkondo wa pili wa wawili hao, unataraji kupigwa leo tarehe 25 Februari saa 11:00 jioni  kwenye dimba la Chamazi jijini Dar es Salaam, Namungo akiutumia uwanja huo kama dimba lake la nyumbani.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Mwenyekiti wa Namungo Zidadu amesema maandalizi yamekamilika kwa 95% hivyo wanasubiri muda ufike waumalize mchezo.

“Maandalizi yamekamilika kwa 95% kila sekta, benchi la ufundi na wachezaji wamefanya mazoezi yakutosha. Safari hii tunachezea kwenye uwanja wa Chamazi wa Azam Complex, uwanja unaotupenda kwani hatujawahi kupata matokeo mabaya”.

“Maeneo mengine yote yapo sawa sawa, tunasubiri muda ufike tuingie kwenye eneo la kuchezea”.

Endapo Namungo ikitoka sare ya aina yeyote au kupata ushindi basi itafuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho kwa mara ya kwanza tokea kuanzishwa kwa klabu hiyo na itacheza kutoka kundi D lenye, Pyramids ya Misri, Raja Casablanca ya Morocco na Nkanza ya Zambia.

Ili Primeiro de Agosto ya Angola iweze kufuzu basi inahitaji ushindi wa utofauti wa kuanzia mabao 5 na kuendelea.

 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava