Ijumaa , 11th Nov , 2016

Kikosi cha wachezaji 23 wa Timu ya Taifa ya Tanzania kimeondoka hii leo kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe utakaopigwa Novemba 13 mwaka huu nchini humo.

Boniface Mkwasa - Kocha wa Taifa Stars

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi, Kocha wa Timu hiyo Charles Boniface Mkwasa amesema, amekiandaa vizuri kikosi chake kwa ajili ya kupambana kwani anafahamu mchezo huo hautokuwa mwepesi kutokana na kila timu kujiandaa.

Amesema kwa upande wao watapambana kwani mchezo huo utawasaidia kuweza kuwaweka katika nafasi nzuri ya viwango vya FIFA.

Mkwasa amesema, hakuna mechi rahisi na hawawezi kukata tamaa kwani anaamini kikosi chake kitapambana mpaka dakika ya mwisho.

Amewataka mashabiki wa soka na watanzania kwa ujumla waendelee kuwaunga mkono na pia kuwakumbusha pale wanapoona kuna dosari ili kuhakikisha timu hiyo inazidi kusonga mbele na kufikia mafanikio waliyojiwekea.

Nahodha Mbwana Samatta

Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ni: Makipa  Deogratius Munishi na Aishi Manula, Mabeki ni Erasto Nyoni Michael Aidan, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein na Vicent Andrew.

Viungo wa Kati ni Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamiru Yassin na wale wa pembeni ni ni Shiza Kichuya, Simon Msuva na Jamal Mnyate na washambuluaji ni Ibrahim Ajib, John Bocco, Mbwana Samatta, Elius Maguli, Thomas Ulimwengu na Omar Mponda     .

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Tanzania inatarajiwa kuondoka leo Ijumaa saa 7.15 mchana Novemba 11, mwaka huu kwenda Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ni: Makipa  Deogratius Munishi na Aishi Manula, Mabeki ni Erasto Nyoni Michael Aidan, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein na Vicent Andrew.

Viungo wa Kati ni Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamiru Yassin na wale wa pembeni ni ni Shiza Kichuya, Simon Msuva na Jamal Mnyate na washambuluaji ni Ibrahim Ajib, John Bocco, Mbwana Samatta, Elius Maguli, Thomas Ulimwengu na Omar Mponda     .

Mchezo huu utakuwa na faida zaidi kwa Tanzania kama ikiwafunga Wazimbabwe kwa kuwa itaongeza alama za nyongeza kwa kushinda ugenini.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.

Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Chile, Colombia na Ujerumani.

Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 31 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Senegal (32), Algeria (35), Tunisia (38) na Ghana (45).