Jumatatu , 25th Mar , 2024

Timu ya Taifa ya Tanzania kwa mpira wa miguu kwa Wanaume Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mongolia kwenye mchezo wa FIFA Series 2024 uliochezwa leo Machi 25-2024 kwenye dimba la Olimpiki mjini Baku nchini Azerbaijan.

Magoli ya Taifa Stars yamefungwa na washambuliaji Kelvin Pius John dakika  ya 49,Abdul Suleiman Sopu  mnamo dakika 62 na kiungo Novatus Dismas aliyefunga bao la 3 mnamo dakika ya 79.

Huu ni mchezo wa pili kwa Stars kucheza kwenye michezo ya FIFA Series 2024 baada ya mchezo wa kwanza kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Bulgaria Ijumaa ya Machi 22-2024