Kikosi cha Taifa Stars
Kikosi cha Taifa Stars kinachoongozwa na Nahodha Himid Mao kwa sasa watashuka kilengeni huku wakimkosa beki wao Abdi Banda baada ya kupewa kadi mbili za njano kwenye mechi mbili tofauti wakati wa mashindano haya.
Katika hatua nyingine, msemaji wa klabu ya Simba SC (aliyefungiwa), Haji Manara ametuma salamu za kuitakia mema kikosi hicho mapema asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake wa Instagram kusema anaamini kikosi hicho cha Stars kitafanya vizuri katika mchezo huo na kuwapa furaha watanzania kwa ujumla.
"Kila la kheri timu ya Taifa leo, tunaamini mnao uwezo wa kuishangaza dunia. Lindeni heshima ya taifa hili", aliandika Manara.
Kwa upande mwingine, Taifa Stars wamepata nafasi hiyo baada ya kuongoza kundi A katika hatua ya awali kwenye mashindano hayo ambapo mchezo wake wa kwanza iliwachapa Malawi kwa mabao 2-0 na mechi iliyofuata ilitoka sare ya bila ya kufungana na Angola huku Mauritius wakitoka sare ya mabao 1-1.