Jumatano , 19th Feb , 2025

Klabu ya Singida Black Stars imemshauri aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Patrick Aussems kuanzisha timu yake ili aonyeshe mfano kwenye soka la Tanzania.

Patrick Aussems - Aliyekuwa Kocha wa Singida Black Stars

Singida iyamesema hayo katika taarifa yao waliyoitoa mchana wa leo wakitolea ufafanuzi kauli tata zilizotelewa na kocha huyo aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa mwaka 2024.

Aussems ambaye pia aliwahi kuhudumu katika kikosi cha Simba alisema kuwa uongozi wa Singida umekua na tabia ya kuingilia majukumu kitendo kilichomchukiza na kuamua kuondoka katika klabu hiyo.

“ Aussems hakuwa na sifa ya kuwa kocha mkuu wala kocha msaidizi kwa ligi kuu ya NBC  kwa mujibu wa kanuni za TFF” Uongozi wa Singida BS FC