Jumapili , 1st Feb , 2015

Michuano ya Kombe la Taifa ya wanawake imezidi kuleta msisimko na kuibua vipaji vipya kutoka nje ya jiji la
Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya soka la wanawake Tanzania, Blasi Kiondo amesema hapo awali walikuwa wakidhani vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake vipo Dar es salaam pekee hususani katika timu ya Taifa ya Twiga Stars lakini wanaamini kama michuano hii itaendelea kuboreshwa itaibua vipaji vingi zaidi hapa nchini.

Kiondo amesema, licha ya kupata timu zilizoendelea hatua ya mbele, lakini wanaamini hata wale walioshindwa hawajashindwa kwa sababu sio wazuri katika mchezo bali ni ushindani uliopo katika kila timu kutaka kufika mbali zaidi na anaamini walioshindwa bado wana vipaji na wana uwezo wa kuitangaza nchi kwa upande wa soka la wanawake.