Jumanne , 10th Aug , 2021

Mlinzi wa Manchester City, Jones Stones amesaini Mkataba wa miaka mitano ili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.

John Stones akiwa katika majukumu yake na klabu yake ya Manchester City

Mkataba baina ya raia huyo wa Uingereza na Manchester City ulikuwa umalizike mwakani lakini sasa atasalia Etihad hadi 2026.

Ilidhaniwa kuwa nafasi ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ilikuwa mashakani baada ya usajili wa Ruben Diaz na uwepo wa Aymeric Laporte lakini akashangaza wengi kwa kiwango alichokionyesha msimu uliopita.

Tangu ajiunge na matajiri hao akitokea Everton kwa dau la paundi milioni 47.5,Stones amecheza michezo 168, huku akishinda mataji yote katika ardhi ya Uingereza.