
Huo ni mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Uganda utakaochezwa Machi 24, 2023 Uwanja wa Suez Canal, Ismailia, Misri.
Kocha huyo amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo wakiwa wapo imara kutokana na maandalizi ambayo wamefanya.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na wachezaji wapo tayari hasa kiakili wanaonekana wapo vizuri.
“Kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo na siwezi kusema sana kuhusu maandalizi kwa kuwa ambacho kinahitajika ni ushindi kwenye mchezo wetu,”.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kambi hiyo nchini Misri ni pamoja na Mbwana Samatta, Feisal Salum, Aishi Manula, Beno Kakolanya