
Mechi kati ya Flying Dribblers dhidi ya Team Kiza
Hayo yameelezwa na katibu mkuu wa shirikisho hilo, Mike Mwita, kwenye mechi za nusu fainali ya kwanza kati ya 'Best of three' zilizopigwa Jumapili ya Julai 29 kwenye uwanja wa taifa wa ndani jijini Dar es salaam.
''Nimepata pongezi nyingi juu ya mashindano yanavyoendelea na kama shirikisho tunavijunia sana mashindano haya ambapo wadau wanatoa maoni mbalimbali na kuweka wazi kuwa ushawishi wa mchezo huu umerejea kutokana na uwepo wa Sprite Bball Kings'' - amesema.
Katibu mkuu wa TBF Mike Mwita
Mike Mwita ni miongoni mwa watu waliojitokeza kushuhudia mechi za hatua ya nusu fainali ambazo zinapigwa kwa mtindo wa 'Best of three' ambapo kwenye mechi za kwanza (Game 1) Flying Dribblers walishinda kwa pointi 84 dhidi ya 70 za Team Kiza huku Mchenga Bball Stars wakishinda kwa pointi 70 kwa 54 za Portland.
Mechi za pili za nusu fainali za michuano hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Sprite, zitapigwa jumamosi hii Agosti 4 kwenye uwanja wa taifa wa ndani. Bingwa atapokea kiasi cha shilingi milioni 10, makamu bingwa akichukua milioni 3 na MVP akitwaa milioni 2.