Southgate lawamani Sancho kukaa benchi

Jumapili , 20th Jun , 2021

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza,Gareth Southgate yupo kwenye lawama nzito juu ya kutomtumia hadi sasa kiungo wake wa pembeni Jadon Sancho.

Kocha Gareth Southgate wa Uingereza

Timu ya taifa ya Uingereza imeshacheza mechi mbili hadi sasa za kundi D , wameshinda wameshinda moja dhidi Croatia 1-0 na suluhu ya 0-0 katika mchezo wa pili dhidi ya mahasimu wao wakubwa Scotland

Sancho ambaye anacheza katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, yupo katika kiwango bora kwa sasa lakini Southgate bado hajampa nafasi ya kuingia uwanjani, kinyume chake amekuwa akimpa kinda mwenzake Jude Bellingham wanaocheza klabu moja.

Mjadala mkubwa wa kwanini Sancho hapewi nafasi ya kucheza huwenda unachagizwa na matokeo ya mchezo wa pili waliotoka sare dhidi ya Scotland.

Maoni yamekuwa mengi juu ya kwanini Sancho hapati nafasi ya kucheza, wengi wameshauri kama kuna uwezekano ni bora amuweke nje nahodha wake Harry Kane ili winga huyu apate nafasi,kuliko kuendelea kumuamini Kane ambaye hana mchango

Wayne Rooney ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo , naye ametoa mawazo yake kwa kile kinachoendelea ndani ya timu ya taifa ya Uingereza akiamini Jack Grealish na Jadon Sancho wanastahili kuanza badala ya Phil Foden

Takwimu za Jadon Sancho akiwa na timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama ‘’Three lions’ aliyoanza kuitumikia mwaka 2018 amecheza mechi 19 ameifungia goli 3 hadi sasa.