Jumatano , 22nd Jun , 2016

Kiungo mpya wa Simba, Mzamilu Yasin aliyetokea Mtibwa Sugar ametamba kuwa suala la kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo halina tatizo na wala hatishwi na uwepo wa Jonas Mkude katika nafasi hiyo.

Kiungo huyo aliyesajiliwa hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili pia alieleza atajitolea zaidi kuisaidia Simba msimu ujao ili irejee kwenye njia yake na kukata kiu ya makombe klabuni hapo.

Aidha Mzamilu aliongeza kuwa kuwa hatishwi na uwepo wa viungo wengi klabuni hapo akiwemo Justice Majabvi, Said Ndemla, Awadh Juma, Mwinyi Kazimoto, Peter Mwalyanzi na Mkude kwa kuwa yeye ni mpambanaji na anaiamini kazi yake.

Pia alisema kuwa anauwezo wa kucheza nafasi zote za viungo ila anaipenda zaidi namba nne hivyo hana hofu ya namba kwenye kikosi cha kwanza.