Taarifa ya klabu hiyo leo imeeleza kuwa Kutinyu ambaye ni raia wa Zimbabwe ameungana na kikosi kilichosafiri kwenda Mwanza kwaajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC siku ya Jumatano.
Kutinyu ambaye alikuwa nchini kwao Zimbabwe kwaajili ya matibabu amerejea nchini baada ya kukamilisha matibabu yake na yupo tayari kuitumikia timu yake.
Kiungo huyo mshambuliaji alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kupata majeraha aliyoyapata wakati wa mchezo wa Kombe la shirikisho (FA) ulioikutanisha Singida United na Bodaboda FC ya Arusha.
Singida United inashika nafasi ya nne ikiwa na alama 30 kwenye michezo 16 huku wapinzani wao Mbao FC wakiwa katika nafasi ya saba wakiwa na alama 18 baada ya michezo 16.

