Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam imeondoka leo kuelekea Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara Mzunguko wa pili.
Akizungumza na East Africa Radio,afisa habari wa timu hiyo,Humphrey Nyasio amesema timu hiyo imeondoka na kikosi cha wachezaji wote pamoja na wale waliowasajili msimu wa Dirisha dogo la usajili.
Nyasio amesema timu hiyo inatarajia kufanya mazoezi visiwani humo kwa muda wa siku tatu ambapo inatarajiwa kurejea jijini kwa ajili ya kujiandaa na mechi mbalimbali zinazowakabili.