Alhamisi , 31st Dec , 2015

Simba imefanikiwa kupangua ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza Januari 1, 2016 Zanzibar baada ya timu hiyo kukabiliwa na mchezo wa kiporo wa Ligi ya soka Tanzania Bara.

Simba imefanikiwa kupangua ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza Januari 1, 2016 Zanzibar baada ya timu hiyo kukabiliwa na mchezo wa kiporo wa Ligi ya soka Tanzania Bara.

Simba inatarajiwa kucheza na Ndanda Mchezo huo wa Ligi Kuu utapigwa ugenini kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kesho januari mosi 2016.

Katika ratiba hiyo ya kombe la Mapinduzi Simba ilipangwa kushuka dimbani Januari 2, kwa kupambana na Jamhuri kuanzia saa 2 usiku kwenye uwanja wa Amani, lakini imekuwa ngumu kwasababu ya uchovu wa wachezaji wao utakao tokana na ugumu wa mechi ya Ndanda na safari ya kutoka Mtwara hadi Zanzibar.

Msemaji wa Simba Hajji Manara amesema wamefurahi ombi lao kukubaliwa na chama cha soka ZFA, na wamejipanga kuhakikisha wanacheza vizuri mashindano hayo na kutetea ubingwa wao walioutwaa msimu uliopita.