Simba Wanawake waingia Ligi Kuu

Thursday , 12th Oct , 2017

Klabu ya Simba ya wanawake alimaarufu kama Simba Queens leo Oktoba 12, 2017 imefanikiwa kupanda daraja na kuingia Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania msimu wa 2017/2018 baada ya kuifunga klabu ya Tanzanite kwa magoli 3-0. 

Wachezaji wa Simba Queens wakifurahia kupanda Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Klabu ya Simba Queens ambayo ilikuwa ikishiriki Ligi ndogo ya wanawake pamoja na klabu ya Alliance Queens zimefanikiwa kupanda daraja na sasa zitacheza Ligi Kuu ya wanawake Tanzania kwa msimu 2017/2018. 

Kufuatia hatua hiyo mashabiki wa Simba wameipongeza timu yao hiyo ya wanawake kuweza kufanikiwa kuingia Ligi Kuu ya Wanawake kwa msimu wa 2017/2018.