Jumatano , 16th Apr , 2014

Katika Juhudi kuhitimisha ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa heshima, kikosi cha klabu ya Simba kimeondoka hii leo jijini Dar es salaam kuelekea visiwani Zanzibar kupiga kambi kujiandaa na pambano dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

Mashabiki wa Simba wakiangalia moja ya mechi za timu hiyo,jijini Dar es Salaam.

Katika Juhudi kuhitimisha ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa heshima, kikosi cha klabu ya Simba kimeondoka hii leo jijini Dar es salaam kuelekea visiwani Zanzibar kupiga kambi kujiandaa na pambano dhidi ya watani zao wa jadi Yanga mchezo utakaopigwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Afisa habari wa klabu hiyo, Bi. Aisha Muhaji amesema msafara huo una wachezaji 18 na viongozi watatu wakiongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji Said Pamba pamoja na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Logarusic pamoja na msaidizi wake Suleiman Matola.

Muhaji amesema miongioni mwa wachezaji waliomo katika kikosi hicho ni pamoja na magolikipa Ivo Mapunda na Yaw Berko na wengine ni Joseph Owino, Donald Musoti, Issa Rashid (baba ubaya), Wiliam Lusian Gallas, Ramadhani Singano Messi, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Said Nassoro Cholo, Henry Joseph, Abdulhalim Humud, Awadh Juma, Uhuru Selemani, Zahoro Pazi, Amri Kiemba, Amis Tambwe na Said Ndemla.

Wakati Simba ikielekea Zenji, watani zao Yanga wamewasili leo DSM kutoka mkoani Kilimanjaro, na bado hawajaweka wazi mustakabali wa kambi yao.