Jumanne , 10th Oct , 2023

Ligi kuu soka Tanzania bara imesimama kupisha kalenda ya kimataifa ya FIFA kupisha timu za taifa zicheze michezo ya kirafiki na mashindano. Hizi ni baadhi ya takwimu za michezo ya Ligi Kuu iliyochrzwa mpaka sasa Ligi ikiwa imesimama baada ya michezo ya roundi ya 5 kukamilika.

Simba SC ndio timu pekee iliyoshinda michezo yote mitano (5) ikiwa na wastani wa ushindi wa asilimia 100 (100%) na ndio vinara wa Ligi wakiwa na alama 15 kwenye michezi hiyo wamefunga mabao 14 na wamefungwa mabao 4.

 

    Ni timu tatu ndio ambazo bado hazijashinda mchezo hata 1 katika michezo 5 iliyochezwa mpaka sasa. Timu hizo ni Coastal Union ya Tanga wamefungwa michezo 3 sare 2 wana alama 2 wapo nafasi ya 16, sawa na Mtibwa Sugar nao wana alama 2 wapo nafasi ya 15. Namungo FC nao hawajaonja radha ya ushindi wamefungwa michezo 2 sare 3 wana alama 3. 

 

    Yanga SC ndio timu iliyofunga mabao mengi, timu ya wanachi imefunga mabao 15, na wamefungwa goli 1 kwenye michezo yote 5 waliyocheza.

 

    Yanga na Azam FC ndio timu zilizoshinda michezo mingi kwenye viwanja vya nyumbani, timu zote zimecheza michezo 3 na wameshinda michezo yote wamekusanya alama 9 kwenye viwanja vyao vya nyumbani.

    Na Simba SC ndio timu iliyoshinda michezo mingi ugenini. Simba imeshinda michezo yote ya ugenini michezo 3. Katika alama zao 15 alama 9 wamezipata kwenye viwanja vya ugenini.

 

Ligi kuu itaendelea tena Oktoba 23,2023. Baada ya kumalizika kwa kalenda ya kimataifa ya FIFA na michezo inayofuata yay a raundi ya 6.