Jumapili , 23rd Nov , 2014

Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imekanusha taarifa za kusitisha mkataba na kocha wake Patrick Phiri.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa Klabu hiyo Humphrey Nyasio amesema klabu hiyo bado ina mkataba na kocha na amesafiri kwa ajili ya likizo ya wiki moja na atarudi nchini kwa ajili ya kuendelea na programu ya mazoezi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya Nani Mtani Jembe.

Nyasio amesema itaingia kambini na kuendelea na mazoezi huku ikiwa chini ya kocha msaidizi,Suleiman Matola ambapo kocha atawasili nchini na kuendelea na programu yake.