Ijumaa , 28th Mei , 2021

Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni,leo inajitupa uwanjani katika mchezo wa mwisho wa mashindano ya BSAFCON 2021.

Timu ya Tanzania ya soka la ufukweni inayoshiriki BSAFCON2021 nchini Senegal

Tanzania itashuka dimbani dhidi ya Misri ijumaa hii ya tarehe 28/05/2021 katika mchezo ambao mshindi atachukua nafasi ya 5 na atakaye poteza atachukua nafasi ya 6,hii inatokana na timu hizi kumaliza katika nafasi za tatu za makundi yao na kukosa nafasi ya kucheza nusu fainali

Tanzania ilikuwa kundi A akiwa na nataifa ya Senegal na Uganda, huku Misri wakiwa kundi B na Morocco itapanga nafasi za washiriki hawa wawili kama ni 5 au 6, kwa kuwa wameshatolewa kwenye mbio za ubingwa na ushindi wa tatu.

Ratiba inaonesha nusu fainali zitapigwa leo kati Senegal dhidi ya Morocco na nusu fainali ya pili ni Uganda dhidi Msumbiji ambapo mechi hizi zitaweza kupanga mshindi wa kwanza hadi wa 4 kisha mechi ya Tanzania na Misri ikatoa no 5 na 6 pia timu zitakazo fuzu kucheza fainali moja kwa moja zitakuwa zimejikatia tiketi ya kuiwakilisha Africa katika michuano hii kwa ngazi ya dunia inayotarajia kufanyika mwezi wa 8 nchini Urusi