Jumatano , 12th Aug , 2020

Klabu ya Sevilla ya Hispania itaumana na Manchester United kwenye mchezo wa nusu Fainali ya michuano ya Europa itakayopigwa siku ya Jumapili huko Jijini Dusseldorf Nchini Ujerumani.

Mlinda mlango wa Klabu ya Manchester United akiokoa mkwaju wa aliyekua nyota wa Sevilla, Luis muriel katika moja ya mchezo wa michuano ya Ulaya waliyokutana.

Sevilla ambao ni mabingwa mara tano wa michuano hiyo, wametinga nusu fainali baada ya kuifunga Wolves bao 1-0 katika Robo Fainali,shukrani kwa nyota wake Lucas Ocampos aliyepachika bao hilo dakika ya 88 ya mchezo.

Ikumbukwe Manchester United ilitangulia kufika hatua hiyo baada ya kuinyuka Fc Copenhagen kwa bao 1-0 lililofungwa na Bruno Fernandes kwa mkwaju wa penati.

Kwa upande wa Shaktar Donetsk iliifunga Fc Basel kwa bao 4-1 yaliyofungwa na Junior Moraes, Taison Taison, Allan Patrick, na Dodo huku la kufutia machozi la kwa wapinzani lilifungwa na Rick Van Wolfsiwinkel.

Kwa ushindi huo, Shaktar itacheza hatua ya nusu fainali Agosti 17 siku ya Jumatatu dhidi ya Inter Milan  ambayo ilitinga hatua hiyo kwa kuiondosha Bayer 04 Leverkusen kwa bao 2-1.