Alhamisi , 1st Jul , 2021

Winga wa kimataifa wa England Jadon Sancho atakuwa mchezaji wa pili mwenye thamani kubwa katika historia ya taifa hilo endapo kama usajili wake wa kujiunga na Manchester United akitokea Dortmund kwa ada ya uhamisho ya pauni million 73, zaidi ya billion 233 kwa pesa za Tanzania utakamilika.

Jadon Sancho

Kwa sasa mlinzi wa Manchester United na timu ya taifa ya England Harry Maguaire ndio mchezaji anayeshikilia rekodi yakuwa mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi kwa wachezaji wa England baada ya uamisho wake wa kutoka Leicester City kwenda Manchester United mwaka 2019 ambapo alinunuliwa kwa ada ya pauni million 80 ambayo ni zaidi bilioni 255 kwa pesa za kitanzania.

Inaripotiwa kuwa klabu ya Manchester United na Dortmund zimefikia makubaliano ya kufanya biashara ya mchezaji huyo na Man United wapo tayari kulipa Pauni million 73 ambayo watalipa kwa awamu tano, lakini bado usajili wa mchezaji huyo haujatangazwa rasmi kwa sababu bado hajafanya vipimo vya afya na kufikia makubaliano binafsi na Manchester United juu ya mkataba wake, na kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa kwenye michuano ya Euro 2020.

Sancho mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano (5) ambao utakuwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi. Msimu uliopita alicheza jumla ya michezo 38 alifunga mabao 16 na alitoa pasi za usaidizi wa mabao (assists) 20 kwenye mashindano yote.