Jumatatu , 12th Mei , 2025

Simba SC ndio timu pekee ambayo ina wachezaji Watatu wa safu ya ushambuliaji ambao wamefunga magoli 10+ Ligi Kuu ya NBC.

Leonel Ateba, Steven Mukwala na Jean Ahoua

Simba inakuwa timu pekee na hakuna timu nyingine zaidi yake licha ya Yanga kuwa ndio Timu yenye magoli mengi zaidi Ligi Kuu (68) huku Simba SC wakishika nafasi ya pili kwa magoli 62 tofauti ikiwa ni goli 6.

Jean Charles Ahoua amefunga magoli 15, Leonel Ateba amefunga magoli 12 huku Steven Mukwala naye amefunga magoli 11 na kukamilisha idadi ya wachezaji watatu wa safu ya ushambuliaji wenye magoli mengi zaidi Ligi Kuu msimu huu.

Wachezaji Clement Mzize wa Yanga amefunga magoli 13, Prince Dube Yanga magoli 12, Jonathan Sowah wa Singida Black Stars amefunga magoli 11, Elvis Rupia magoli 10 na Pacome Zouzoua amefunga magoli 9.