
Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalum wa instagram baada ya kupita siku moja tokea nyota huyo wa kimataifa anayechezea klabu ya Real Madrid kuweka hadharani gari hilo katika mtandao wake na kufanya mamia ya watu kumpongeza kwa hatua hiyo aliyofikia huku wengine wakibakia kutoamini kwa kilichotokea.
"Bugatti ya 2017 imenunuliwa na Ronaldo kwa thamani ya Dola milion 1.8, karibia na Bilioni nne za madafu. Unalipa 'salary' ya mwaka mzima kwa wachezaji wa Yanga, Simba na Azam. Huu ni ukatili uliopitiliza", ameandika Manara.