Alhamisi , 29th Feb , 2024

Kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba amefungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka minne kutokana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli yasiyoruhusiwa michezoni.

Pogba mwenye umri wa miaka 30 amesema kila kitu alichokitengeneza kwenye maisha yake ya soka kimeharibika kwa sasa huku kiungo huyo  alisimamishwa kushiriki kwenye soka tangu mwezi Septemba 2023

baada ya kubainika kutumia madawa ya testosterone huku Paul labile Pogba ameitumkia Juventus ndani ya dakika 51 pekee dhidi ya Bologna na Empoli  ndani ya msimu huu huku anataraji kurejea dimbani mwaka 2027 akiwa na umri wa miaka 33 kushiriki kwenye soka