Nyota wa Los Angeles Clippers, Paul George akijaribu kumtoka Chris Paul wa Phoenix Suns.
Ushindi wa Clippers ulichagizwa na uwezo binafsi wa nyota wake, Paul George ambaye alifikisha alama 41, rebaundi 13 na assisti 6 zilizomfanya kuwa nyota wa mchezo kwa kufikisha alama nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote kwenye mchezo huo.
Ni hii ni kwa mara ya pili mfululizo Paul anaibuka kuwa mchezaji nyota wa mchezo wa Clippers dhidi ya Suns lakini pia ni mara ya pili mfululizo kwenye michezo miwili ya mwisho kwenye hatua ya nusu fainali dhidi ya Utah Jazz ambapo pia Kawhi Leonard hakuwepo.
Wafuatiliaji wengi wa mchezo huo waliusubiri mchezo huo kwa hamu kwani Clippers walishafungwa kwenye michezo 2-0 mfululizo na kupata ushindi mmoja kwenye mchezo wa mzunguko watatu.
Clippers walifungwa tena kwenye mzunguko wa nne mpaka kufikia hapo jana ambapo wangefungwa basi wangeondoshwa na kushuhudia Suns kuwa mwabingwa wa ukanda huo.
Gumzo lingile lilikuwa majeraha ya nyota tegemezi kikosini, Kawhi Leonards anayesumbuliwa na maumivu ya nyong na wengi kuhisi huenda Clippers wangeondoshwa alfajiri ya kuamkia leo lakini haikuwa wote.
Paul alipata upinzani mkali kutoka kwa kijana Devin Booker aliyeonesha kiwango safi kwa kupata alama 31, rebaundi 4 na assisti 3 ambazo hazikutosha kuwapa ushindi. Wawili hao wanatazamiwa kucheza tena Julai 1, 2021 kutafuta bingwa wa fainali hiyo.
Ligi hiyo itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho ambapo timu ya Milwaukee Bucks itakipiga na Atlanta Hawks saa 10 Alfajiri ya kesho kwenye mchezo wa mzunguko wa 4 wa fainali ya NBA kwa ukanda wa mashariki.

