Jumatatu , 19th Feb , 2018

Hatimaye kijana Adam Abubakary kutoka Bukoba mkoani Kagera aliyejizolea umaarufu kwa jina la ''Okwi wa Bukoba'' baada ya kuonekana akiwa amechora jina la Okwi kwenye fulana yake amekabidhiwa jezi rasmi ya Emmanuel Okwi.

Okwi huyo wa Bukoba amekabidhiwa jezi hiyo leo kwenye moja ya tawi la Simba huko Bukoba kazi iliyosimamiwa na kiongozi wa makundi ya kwenye mitandao ya mashabiki wa klabu hiyo J-Munyama.

Kijana huyo ambaye ni shabiki wa Simba SC alionekana Februari 11 mwaka huu wakati wa mchezo wa ligi kuu kati ya Kagera Sugar na Azam FC na kujitambulisha kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Simba SC na amapneda Okwi.

Okwi ambaye ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu akiwa amefunga mabao 14 hadi sasa anavaa jezi namba Saba ndani ya Simba pamoja na timu ya taifa ya Uganda.