Alhamisi , 29th Sep , 2016

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi kitakachosafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.

Charles Boniface Mkwasa

Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.

Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:

Makipa
Deogratius Munishi – Young Africans
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC

Mabeki
Shomari Kapombe – Azam FC
Juma Abdul – Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
David Mwantika - Azam FC
James Josephat – Tanzania Prisons

Viungo wa Kati
Himid Mao - Azam FC
Mohammed Ibrahim – Simba SC
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC

Viungo wa Pembeni
Shiza Kichuya – Simba SC
Simon Msuva - Young Africans
Juma Mahadhi - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba
Hassan Kabunda – Mwadui FC

Washambuliaji
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli – Oman
Thomas Ulimwengu – TP Mazembe Congo

Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.