Alhamisi , 4th Jun , 2015

Klabu ya Mwadui ya mkoani Shinyanga imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Paul Nonga na kiungo Anthony Matogola kutoka klabu ya Mbeya City.

Nonga na Matogola wametua katika klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu ambapo Nonga amemaliza mkataba wake katika klabu ya Mbeya City.

Matogola aliyesaini mwaka mmoja katika klabu hiyo amesajiliwa na Mwadui mara baada ya mazungumzo ya pande zote mbili kukamilika.

Mwadui iliyopo chini ya kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Julio Kihwelu itacheza katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao mara baada ya kufanikiwa kupanda daraja msimu huu kuingia kunako ligi hiyo