Alhamisi , 25th Feb , 2016

Kijana mdogo aliyeonesha kumkubali Messi, kwa kuvaa mfuko wa plastiki wenye jina la Mess na namba 10, hatimaye amepewa jezi halisi ya dukani.

Mtoto mmoja nchini Afghanistan ambaye aligonga vichwa vya mitandao ya kijamii alipovaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Argentina.

Murtaza Ahmadi mwenye umri wa miaka 5, anatoka katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

Timu ya usimamizi wa Messi ilithibitisha siku ya Alhamisi kwamba Murtaza alitumiwa jezi ya mshambuliaji huyo wa Argentina iliotiwa saini pamoja na mpira kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona ambaye ametuzwa kuwa mchezaji bora mara tano.

''Ninampenda Messi na fulana yangu inasema Messi ananipenda", Murtaza alisema, huku akimuigiza mshambuliaji huyo anavyoshangilia bao lake.

Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na picha moja iliyoenea katika mitandao ikimuonesha amevaa fulana ya plastiki ya Messi.