Amesema msimu uliopita hawakufanya vizuri sana kwenye safu hiyo na kushindwa kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa na kuishia kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.
-
Simba msimu uliopita wa 2023/24 walifunga jumla ya mabao 59 na kufungwa 25 tofauti na 2022/23 ambao walifunga mabao 75 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 17, kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
-
Kazi kubwa ambayo anaifanya Kocha Fadlu ni kuwapa mbinu washambuliaji wakiongozwa na Kibu Denis, Freddy Michael, Steven Mukwala na Joshua Mutale mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.
-
Matola ameiambia EATV kuwa kocha Fadlu anapita katika njia ya Simba ambao makocha waliofanikiwa kipindi cha timu hiyo ilipofanikiwa na tangu amekabidhiwa anasisitiza zaidi washambuliaji kuwa makini wanapokuwa uwanjani.
Jumapili , 21st Jul , 2024
Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola ameeleza kuwa tatizo la ufungaji ndani ya timu hiyo limepata mwarobaini baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davids kuwapa washambuliaji Programu maalum ya namna ya kufunga kwa ajili ya msimu ujao.