Mohamed Ally enzi za upiganaji wake akiwa amemwangusha mmoja wa wapinzani wake wakati huo.
Umati mkubwa wa waomblolezaji unataraji kuhudhuria mazishi ya nguli wa masumbwi duniani Muhammad Ali yatakayofanyika ijumaa iajyo na kila mtu akipewa nafasi ya kumwaga nguli hiyo.
Mazishi ya nguli huyo yatafanyika katika mji aliozaliwa wa Louisville, Kentucky huku rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton akiwasilisha ujumbe maalumu wa maombolezo hayo.
Baadhi ya watu maarufu nao watahudhulia mazishi hayo wakiwemo mchekeshaji maarufu nchini humo Billy Crystal na mwandishi nguli wa michezo Bryant Gumbel nao wakitarajiwa kuzungumza pia.
Nguli huyo wa masumbwi uzito wa juu duniani amefariki ijumaa ya wiki hii akiwa na umri wa miaka, 74, kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi.
Pamoja na mazishi yake kufanyika Ijumaa ijayo lakini kabla ya siku hiyo yaani Alhamis kutatanguliwa na shughuli binafsi za familia yake.
Bingwa huyo mara tatu wa uzito wa juu duniani na mmoja wa watu maarufu kabisa duniani kuwahi kutokea alifariki huko Phoenix, Arizona, na mwili wake utapelekwa mjini Kentucky siku mbili zijazo.
Na anataraji kuzikwa katika makaburi ya nyumbani kwao [Cave Hill Cemetery] huko Louisville, mji ambao alizaliwa nguli huyo mnamo mwaka 1942.
Nguli huyo atafanyiwa dua maalumu mchana ikihudhuliwa na zaidi ya watu elfu ishiriki ikifanyika katika eneo la KFC Yum Center, dua itakayoendeshwa kwa utamaduni wa kiislam kutokan na imani ya marehemu huyo.