Ijumaa , 30th Jul , 2021

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya klabu ya Simba, Mohammed Dewji haitmaye amekabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni ishirini ikiwa ni thamani ya asilimia 49 ya hisa katika kuwekeza ndani ya klabu hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni 20 leo hii Julai 30, 2021 mbele ya Mdhamini, Mwenyekiti wa klabu hiyo mbele ya Wanahabari.

Mo Dewji amekabidhi hundi hiyo kwa Mdhamini Mkuu wa klabu hiyo, Adam Mgoyi na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Muhtaza Mangungu ambaye pia ni mbunge wa Kilwa kupitia chama cha Mapinduzi CCM mbelel ya Wanahabari saa sita mchana wa leo Julai 30, 2021.

Baada ya kukabidhi hundi hiyo, Mo amesema anawashukuru wanasimba na watanzania wote kwa ushirikiano wao na kuthibitisha kupewa baraka zote na Tume ya Ushindani 'FCC' kwa kukamilisha mchakato wa ubadilishwaji wa Uendeshwaji wa klabu hiyo wazo lilioanza toka mwaka 2003.

"Nawashukuru Wanasimba na Watanzania wote bila wao tusingekuwa hapa. Tumekamilisha mchakato wa mabadiliko. Tumepata hati kutoka FCC ya kuturuhusu kumalizia mchakato. Ndani ya miaka minne nimetumia bilioni 21.3 (sawa na bilioni 5.3 kila mwaka ) Ilitumika kusajili wachezaji, makocha, pre seasons, mishahara na uendeshaji wa klabu.”

Na hatimaye akathibitisha kuweka kiasi hicho cha pesa mbele ya wanahabari.

"Leo naweka hiyo Bilioni 20 ya hisa asilimia 49 mbele ya mdhamini wa klabu na mwenyekiti wa klabu."

Naye, Mdhamini Mkuu wa Klabu ya Simba, Adam Mgoti amewatoa hofu wanasimba na kusema Utekelezaji wa yale waliyoyapanga kuelekea mabadiliko ya klabu inafikia mwisho.

"Utekeleza wa yale tuliyoyapanga (mabadiliko) unaenda kufikia mwisho”.