Jumanne , 15th Nov , 2022

Kiungo Jonas Mkude wa Simba kesha anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mkude ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Juma Mgunda anatarajiwa kukosekana kutokana na kutokuwa fiti kiafya.

Simba imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu kesho itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Namungo ambao nao wanazihitaji pia pointi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kocha  Mgunda amesema:”Mkude ni mgonjwa hayupo vizuri kwa sasa pia hata John Bocco yeye alikuwa ni mgonjwa ameanza mazoezi taratibu,”.

Kwenye ligi Mkude katupia bao moja ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.