Jumatano , 17th Dec , 2014

BONDIA Francis Miyeyusho amewataka waandaaji wa mapambano kuandaa Pambano litakalomkutanisha na Mabondia kutoka nchi za nje ili kuendeleza kukuza kipaji chake zaidi.

Bondia Francis Miyeyusho

Akizungumza na East Africa Radio, Miyeyusho amesema hakuwa na matarajio ya kukutana na Bondia kutoka hapa nchini Tanzania lakini anatamani siku moja kupanda ulingoni na Bondia Fadhili Majiha katika Pambano la kumaliza Ubishi.

Miyeyusho amesema hivi sasa hana pambano lolote lakini anaendelea na mazoezi kwa ajili ya kuzidi kujiimarisha kwa ajili ya mapambano mbalimbali ya mwakani ambayo anaami atafanya vizuri kutokana na mazoezi anayoendelea nayo hivi sasa.

Miyeyusho amesema mpaka sasa anaamini yeye ni Bondia Bora kwani katika Pmano la mara ya mwisho alikutana na Bondia Mohamed Matumla ambapoi alimpiga hivyo kutokana na pambano lake hilo na mengine mengi aliyopigana anaamini hakuna Bondia wa hapa nchini atakayeweza kupanda naye Ulingoni na kupambana naye kwa sababu anaamini atamp[iga lakini hatakuwa ameonyesha kipaji chake.