Alhamisi , 27th Aug , 2015

Michuano wazi ya mchezo wa Gofu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 29 mpaka 30 Uwanja wa Lugalo jijini Dar es salaam kwa kushirikisha wachezaji takribani 200 kutoka vilabu mbalimbali na wachezaji binafsi.

Akiuzungumza jijini Dar es salaam, Msemaji wa Klabu ya Gofu ya Lugalo John Nyalusi amesema, mashindano hayo yatashirikisha wachezaji wa umri mbalimbali kuanzia vijana wenye Umri wa chini ya miaka 9, chini ya miaka 18 na wenye Umri wa miaka 60 na kuendelea.

Nyalusi amesema, michuano hiyo yenye lengo la kukuza na kuutangaza mchezo huo zaidi hapa nchini na kuweza kupata wachezaji wengi vijana utazinduliwa rasmi na Mkuu wa Majeshi wa nchini Afrika Kusini.