Alhamisi , 29th Mei , 2014

Michael Wambura leo amewasilisha rufaa kupinga kuenguliwa kwake kwa kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF akiwa na vielelezo zaidi ya 14 vya kutetea hoja yake akipinga maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba

Michael Wambura kushoto akizungumza jambo katika moja ya mikutano yake.

Mgombea nafasi ya Urais wa Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam aliyeondolewa katika mchakato wa uchaguzi Michael Wambura amewasilisha rufaa ya kuenguliwa kwenye uchaguzi huo katika kamati ya rufaa ya uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF)

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuwasilisha rufaa yake, Wambura amesema ameamua kukata rufaa na kuiwasilisha katika ngazi hiyo ya kamati ya uchaguzi ya TFF kwa kuwa anaamini hajatendewa haki katika ngazi ya chini na anaamini kamati zitakaa katika muda muafaka na kumtendea haki mapema iwezekanavyo

Aidha Wambura amesema rufaa yake imezingatia misingi ya kisheria ikifuata katiba ya simba, katiba ya TFF, na sheria mbalimbali zinazotawala mchezo wa soka na mambo yanayohusiana na chaguzi za soka hapa Tanzania.