Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia tovuti yake rasmi inasema ripoti za kitabibu zimeonesha kuwa Mbappe amepata maumivu ya misuli ya paja kwenye mguu wake wa kushoto, hivyo ataikosa michezo kadhaa ikiwemo dabi ya Madrid dhidi ya Atletico Madrid, mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Lille na Real Valladolid.
Katika mchezo wa La Liga dhidi ya Deportivo Alaves Mbappe alionekana kuchechemea dakika chache kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Arda Guller dakika ya 80
Akiwa Real Madrid mshambuliaji huyo tayari amepachika mabao 5 katika mechi 7 za ligi kuu ya Hispania alizocheza.