
Miyeyusho anayecheza uzito waFeatherweight amesema alipoteza pambano hilo kwa kile kinachoaminika upendeleo wa majaji kwa bondia mwenyeji na kukosa maelekezo kwa mkufunzi wake ambaye hajaambatana naye.
Mabondia wengi wa Tanzania wamekuwa wakisaini mikataba ya nje na kuelekea huko bila ya wakufunzi wao,na mwisho wa siku huishiwa kudundwa.
Bondia Nasibu Ramadhani anayecheza uzito wa Bantam naye alikuwa nchini Namibia Novemba mwaka uliopita,kucheza mkatanda wa WBO Afrika uzito mwepesi lakini alipoteza pambano hilo kwa pointi