Bwire amesema kuwa alialikwa kupata ftari lakini alilazimika kurudi baada ya kujikuta akiwa amevalia tofauti na wenzake, ambapo aliaondoka kwa masikitiko huku akiwa na hamu ya kufuturu
“Jana nilialikwa mahala kufuturu, lakini nilipofika eneo la shughuli, kila niliyemuona, kavaa kanzu, mie vazi langu, suruali na shati. Kanzu sina, sijawahi hata kuulizia bei, kwa mazingira hayo, nikaogopa kuwa kituko, nikalazimika kutii amri ya Jeshi, 'nyuma geuka'.”, ameandika Bwire.
Bwire ameongeza kuwa leo amealikwa mahala fulani, na anaaona mchezo utakuwa ule ule kwani vazi rasmi kanzu hana na kuomba msamaria mwema ajitokeza kumpatia.